Serikali ya Marekani imeanza kutekeleza mpango wa kuhamisha baadhi ya ndege zake zilizokuwa zikitumika nchini Israel kwenda katika vituo vya kijeshi vilivyoko barani Ulaya, hatua inayokuja wakati hali ya usalama katika Mashariki ya Kati ikiendelea kuzua wasiwasi mkubwa kwa jumuiya ya kimataifa.........................TAZAMA VIDEO.
Kwa mujibu wa taarifa zilizoripotiwa na vyombo mbalimbali vya habari vya kimataifa, operesheni hiyo ya kuhamisha ndege inatarajiwa kufanyika ndani ya kipindi cha saa 72.
Kwa mujibu wa taarifa zilizoripotiwa na vyombo mbalimbali vya habari vya kimataifa, operesheni hiyo ya kuhamisha ndege inatarajiwa kufanyika ndani ya kipindi cha saa 72.
Hatua hiyo imeelezwa kuwa sehemu ya maandalizi ya kijeshi yanayolenga kulinda vifaa muhimu vya Marekani huku vikibaki tayari kutumika haraka iwapo hali ya usalama katika eneo hilo itazidi kuzorota.
Vyanzo vya kiusalama vimeeleza kuwa ndege zinazohamishwa zinatoka katika maeneo mbalimbali ya kijeshi yaliyoko Israel.
Vyanzo vya kiusalama vimeeleza kuwa ndege zinazohamishwa zinatoka katika maeneo mbalimbali ya kijeshi yaliyoko Israel.
Baada ya kuwasili Ulaya, ndege hizo zitawekwa katika vituo vinavyoweza kutumika kwa haraka kwa shughuli za kijeshi au za usalama endapo kutatokea mabadiliko makubwa ya ghafla katika mazingira ya kikanda. SOMA ZAIDI.
Post a Comment