Aliyetabiri Matukio Ya Oktoba 29 Aibuka Tena, Atoa Ujumbe Mzito Kuhusu Tanzania

Tafadhali Zingatia: Ikiwa unasoma kwenye PHOENIX, tafadhali bofya kitufe cha “Soma Makala Asili” kilicho upande wa juu kulia ili kusoma makala kamili.

Dar es Salaam. Nabii Rolinga amezikamata tena hisia za wengi baada ya kutoa kauli mpya kufuatia kurejea nchini Zimbabwe akitokea Tanzania. Katika maelezo yake, amesema bado ana matumaini makubwa kwa Tanzania licha ya changamoto mbalimbali zinazoendelea kujitokeza.

Akizungumza baada ya safari yake, Rolinga alirejea kuelezea tukio la kiroho alilolifanya kabla ya kuondoka nchini, akihusisha kitendo cha "kuugongesha glasi" na ujumbe aliokuwa ameubeba kwa taifa. Amesema tukio hilo halikuwa la kawaida bali lilikuwa sehemu ya kile alichodai kuwa ni ishara ya maono yake.

Katika kauli yake, Rolinga alisisitiza kuwa anaamini hakuna damu yoyote iliyomwagika bila haki ambayo haitapata haki yake kwa wakati unaofaa. Amesema pamoja na hali mbalimbali zinazoendelea kujitokeza, bado anaona Tanzania ikiwa na amani, matumaini na utulivu.

Aidha, ameongeza kuwa kwa mtazamo wake, kipindi cha majaribu kinachoonekana sasa kitapita, na taifa litaendelea kuwa salama huku akieleza imani yake kuwa mwisho wa yote mambo yatakuwa sawa.Endelea Kusoma Kwa Kubofya Hapa.

Post a Comment

Previous Post Next Post