Mjadala kuhusu video inayodaiwa kumhusisha mwanafunzi wa Kidato cha Tatu na kusambaa kwa kasi kwenye mitandao ya kijamii umeendelea kuchukua sura mpya baada ya taarifa zinazodai kuwa mwanaume anayetajwa kuhusika katika tukio hilo naye ni mwanafunzi.
Kwa mujibu wa taarifa iliyochapishwa na ukurasa wa Official Mkali Wenu, baadhi ya watu wameanza kutoa maelezo mapya kuhusu mwanaume anayedaiwa kuonekana kwenye video hiyo, wakidai kuwa kijana huyo pia ni mwanafunzi.
Taarifa hiyo imeeleza kuwa, kwa mujibu wa kaka wa msichana anayezungumziwa, mwanaume huyo anatajwa kuwa mwanafunzi mwenzake. Hata hivyo, madai hayo bado yanahitaji uthibitisho kutoka kwa mamlaka husika kabla ya kuchukuliwa kuwa ukweli.
Katika maelezo mengine yanayosambazwa kwenye mitandao, msichana huyo anadaiwa kusema kuwa mwanaume huyo alikuwa na simu na alimwambia aache kurekodi kwa madai kuwa Mama Samia akiona video hiyo atamfungua.
Kauli hiyo imeongeza maswali mengi miongoni mwa watumiaji wa mitandao ya kijamii, ambao wameendelea kujadili mazingira ya tukio hilo na kutaka ukweli ujulikane.
Awali, Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu, Dorothy Gwajima, aliingilia mjadala huo kwa kutoa ujumbe akitaka kufahamu shule anayosoma mwanafunzi anayezungumziwa ili kushirikiana na walimu katika hatua za kumsaidia.
Waziri huyo alisisitiza kuwa hataki kutumiwa video hiyo wala kupewa maelezo mengi, bali anahitaji suala hilo lifuatiliwe kwa kuzingatia Sheria ya Mtoto.

Post a Comment