“Kesho Tutafanya Maamuzi ya Mwisho,” Wajumbe wa CUF Wasema Huku Hatima ya Profesa Ibrahim Lipumba Ikitikiswa Kabla ya Uchaguzi Mkuu wa Februari 21, 2026

Mvutano ndani ya Chama cha Wananchi (CUF) umefikia hatua nyeti, huku hatima ya uongozi wa Profesa Ibrahim Lipumba ikionekana kuwa shakani iwapo mchakato wa kesho utaenda kinyume na matarajio ya upande wake. 

Kesho, Februari 21, 2026, wajumbe wa Baraza Kuu la Civic United Front wanatarajiwa kupiga kura ya kuwachagua viongozi wapya wa chama hicho katika mkutano mkuu wenye mvutano mkubwa.

Hatua hii inafanyika siku chache baada ya Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa kutangaza kutoutambua uongozi wa sasa wa CUF na kuagiza uchaguzi wa mwenyekiti urudiwe. 

Uamuzi huo umeibua mjadala mkali ndani ya chama, huku baadhi ya viongozi wakisema ni kuingilia uhuru wa chama kufanya maamuzi yake ya ndani.

Naibu Katibu Mkuu wa CUF–Bara, Magdalena Sakaya, amesema wazi kuwa hawakubaliani na msimamo wa Msajili na tayari wameamua kupeleka suala hilo mahakamani. Kwa mujibu wake, chama kina katiba na taratibu zake, na uchaguzi ulifanyika kwa kuzingatia kanuni hizo.Kusoma Zaidi, bonyeza hapa.

Post a Comment

Previous Post Next Post