Changamoto za afya ya akili zimeendelea kuwa suala linalozua mjadala mkubwa duniani kote, huku ripoti mpya ikionyesha kuwa asilimia 91 ya wafanyakazi wanaoomba likizo kazini wanakabiliwa na matatizo ya kisaikolojia yanayohusiana na msongo wa mawazo, uchovu wa akili na shinikizo kubwa la kazi.
Takwimu hizo zimeibua wasiwasi kuhusu mazingira ya kazi na namna yanavyoathiri ustawi wa wafanyakazi.
Kwa mujibu wa wataalamu wa afya ya akili, ongezeko la majukumu kazini, matarajio makubwa ya uzalishaji na ukosefu wa muda wa kupumzika ni baadhi ya sababu zinazochangia kuongezeka kwa matatizo hayo.
Kwa mujibu wa wataalamu wa afya ya akili, ongezeko la majukumu kazini, matarajio makubwa ya uzalishaji na ukosefu wa muda wa kupumzika ni baadhi ya sababu zinazochangia kuongezeka kwa matatizo hayo.
Wengi wa wafanyakazi wamekuwa wakilazimika kuomba likizo ili kupata muda wa kurejesha hali yao ya kisaikolojia na kupunguza athari za uchovu wa akili.
Aidha, wataalamu hao wameeleza kuwa tamaduni na desturi za jamii zina nafasi muhimu katika kujenga au kudhoofisha afya ya akili. Mila na imani za kidini mara nyingi husaidia watu kupata faraja na nguvu za kukabiliana na changamoto za maisha.

Hata hivyo, wakati mwingine imani hizo zinaweza kusababisha madhara pale zinapotumika kupuuza mahitaji ya matibabu au ushauri wa kitaalamu.
Mfano wa tukio lililotokea nchini Kenya, ambapo baadhi ya waumini walifunga kwa muda mrefu kwa misingi ya kiimani hadi kusababisha vifo, umetajwa kama onyo la umuhimu wa kuweka uwiano kati ya imani na afya.
Post a Comment