Mji wa Kyela mkoani Mbeya umejikuta ukigubikwa na shamrashamra za kisiasa baada ya viongozi mbalimbali wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kuwasili na kupokelewa kwa hamasa kubwa na wanachama pamoja na wananchi wa eneo hilo.
Miongoni mwa viongozi waliopokelewa ni Mwenyekiti wa CHADEMA Kanda ya Pwani, Boniface Jacob maarufu kama Bon Yai, Mwenyekiti wa BAWACHA Mkoa wa Rukwa na Mbunge Mstaafu wa Nkasi Kaskazini, Aida Khenan, pamoja na Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Mbeya, Masaga Kaloli.

Ujio wao umevutia mamia ya wananchi waliojitokeza kandokando ya barabara na maeneo mbalimbali ya mji huo kuwapa mapokezi makubwa.
Matukio ya mapokezi hayo yameonekana kuonyesha namna ambavyo shughuli za kisiasa zinaendelea kuvuta hisia za wananchi katika maeneo mbalimbali nchini.

Wafuasi wa chama hicho walionekana wakionesha furaha na matumaini makubwa kuelekea mkutano wa hadhara unaotarajiwa kufanyika jioni ya Juni 7, 2026.
Kwa mujibu wa ratiba ya chama, mkutano huo utajadili masuala kadhaa ya kitaifa ikiwemo ajenda ya Katiba Mpya pamoja na kampeni ya "Free Tundu Lissu" ambayo imeendelea kuwa moja ya hoja kuu zinazobebwa na viongozi wa CHADEMA katika mikutano yao ya hadhara.

Masuala ya maendeleo, demokrasia na ushiriki wa wananchi katika mchakato wa uamuzi wa kitaifa nayo yanatarajiwa kupewa nafasi katika mjadala huo.
Post a Comment