Mwenyekiti wa CCM na Serikali ya Mtaa wa Engosowashi, Kata ya Moshono jijini Arusha, Richard Meshaki Laizer, ametangaza kujiuzulu nafasi yake rasmi baada ya kusoma barua ya kuachia wadhifa huo mbele ya wananchi katika mkutano wa mtaa uliofanyika Juni 7, 2026.
Uamuzi huo ameueleza kuwa umetokana na kile alichodai ni kupunguzwa kwa mamlaka ya wenyeviti wa mitaa katika utoaji wa huduma kwa wananchi.
Akizungumza mbele ya wakazi wa Engosowashi, Laizer alisema mazingira ya sasa ya kiutendaji yamekuwa yakimzuia kutekeleza kikamilifu majukumu aliyokabidhiwa na wananchi kupitia uchaguzi.
Akizungumza mbele ya wakazi wa Engosowashi, Laizer alisema mazingira ya sasa ya kiutendaji yamekuwa yakimzuia kutekeleza kikamilifu majukumu aliyokabidhiwa na wananchi kupitia uchaguzi.
Alidai kuwa baadhi ya maelekezo yaliyotolewa na viongozi wa utawala yamebadilisha mfumo wa utoaji huduma katika ngazi ya mtaa, hali ambayo kwa mtazamo wake imeathiri uwezo wa viongozi waliochaguliwa kuwahudumia wananchi kwa ufanisi.
Kwa mujibu wa Laizer, mabadiliko hayo yalianza kuonekana wazi baada ya kutolewa kwa maelekezo mwezi Machi mwaka huu yaliyowazuia wenyeviti wa mitaa kumiliki mihuri ya ofisi.
Kwa mujibu wa Laizer, mabadiliko hayo yalianza kuonekana wazi baada ya kutolewa kwa maelekezo mwezi Machi mwaka huu yaliyowazuia wenyeviti wa mitaa kumiliki mihuri ya ofisi.
Alisema hatua hiyo ilielekeza huduma nyingi za kiutawala kufanyika kupitia watendaji wa mitaa badala ya wenyeviti waliochaguliwa na wananchi.
Ameeleza kuwa utekelezaji wa maelekezo hayo umeongeza changamoto kwa wananchi wanaohitaji huduma mbalimbali za kiutawala.
Kwa maoni yake, mfumo huo umesababisha baadhi ya wakazi kutumia muda mrefu kupata huduma walizokuwa wakizipata kwa urahisi kupitia viongozi wao wa mitaa.
Post a Comment