Top News

Wanawake wafunguka ukatili wa kingono kwenye sekta hii

Wanawake wafanyabiashara wa samaki katika maeneo ya mwambao wa Bahari ya Hindi mikoa ya Tanga, Lindi na Mtwara wamefichua kuwepo kwa unyanyasaji wa kingono wanaokumbana nao katika shughuli zao za kila siku.

Kwa mujibu wa utafiti wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), baadhi ya wanawake wanalazimika kuingia katika mahusiano ya kimapenzi ili kupata samaki au kununua kwa bei nafuu, hali inayochochewa na changamoto za kiuchumi na upungufu wa rasilimali za uvuvi.

Wanawake hao wamesema hali hiyo imekuwa ikiwanyima haki ya kufanya biashara kwa usawa na heshima, huku baadhi wakilazimika kuvumilia vitendo hivyo ili kuendeleza biashara zao.

Wamesema upendeleo katika minada na kwenye vyombo vya uvuvi hutolewa kwa wanawake walio katika mahusiano na wavuvi au manahodha, jambo linalowaathiri hata wale wenye uwezo wa kifedha.

LHRC imebainisha kuwa mabadiliko ya tabianchi yamepunguza upatikanaji wa samaki na kuongeza ushindani, hali inayochangia kukithiri kwa ukatili huo wa kijinsia.

Taasisi hiyo imesisitiza umuhimu wa kuboresha ushiriki wa wavuvi katika maamuzi na kulinda haki za makundi yanayotegemea sekta ya uvuvi ili kuhakikisha mazingira salama na ya usawa kwa wote.

Post a Comment

Previous Post Next Post