Jeshi la Misri limetangaza kuuawa kwa maafisa wake wawili waandamizi wa Kikosi cha Ulinzi wa Mipaka kufuatia mapambano ya kutumia silaha yaliyotokea wakati wa operesheni za kijeshi dhidi ya makundi yaliyotajwa kuwa ya kihalifu katika eneo la kusini mwa nchi hiyo.
Taarifa hiyo imetolewa Alhamisi, Novemba 5, 2026, na msemaji wa jeshi la Misri, Kanali Ahmed Osman Ali, aliyethibitisha kuwa maafisa hao walipoteza maisha wakati wa kutekeleza majukumu yao ya kiusalama.
Kwa mujibu wa taarifa ya jeshi, maafisa waliofariki ni Kanali Ahmed Samir, aliyekuwa Mkuu wa Majeshi katika Kikosi cha Ulinzi wa Mipaka cha Ukanda wa Kusini, pamoja na Luteni Kanali Ahmed Gouda, ambaye alikuwa Mkuu wa Operesheni za kikosi kimoja cha walinzi wa mipaka katika eneo hilo.

Jeshi limeeleza kuwa vifo vyao vilitokana na makabiliano ya risasi kati ya wanajeshi na watu waliotajwa kuwa wahalifu, wakati vikosi vya serikali vikitekeleza majukumu ya kudhibiti shughuli zisizo halali katika maeneo ya jangwani.
Kwa maelezo yaliyotolewa na msemaji wa jeshi, mapambano hayo yalihusishwa na operesheni maalumu inayolenga kukabiliana na uchimbaji haramu wa madini ya dhahabu katika Jangwa la Mashariki mwa Misri.
Kwa maelezo yaliyotolewa na msemaji wa jeshi, mapambano hayo yalihusishwa na operesheni maalumu inayolenga kukabiliana na uchimbaji haramu wa madini ya dhahabu katika Jangwa la Mashariki mwa Misri.
Shughuli hizo zimekuwa zikihusishwa na uwepo wa makundi yenye silaha yanayojihusisha na uchimbaji usioidhinishwa pamoja na mitandao ya uhalifu inayovuka mipaka.
Jeshi limesema operesheni hiyo inalenga kurejesha udhibiti wa maeneo husika, kulinda rasilimali za taifa na kuhakikisha usalama wa watu wanaofanya kazi katika sekta ya madini.
Katika mkutano na waandishi wa habari, jeshi lilieleza kuwa limekuwa likichukua hatua mbalimbali kabla ya kuanza kwa kila awamu ya operesheni, ikiwemo kutoa tahadhari kwa watu waliopo katika maeneo yanayolengwa ili waache shughuli zisizo halali.

Pia limefanya mikutano na viongozi wa makabila na wazee wa maeneo hayo kwa lengo la kupata ushirikiano katika kurejesha utawala wa sheria.
Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa, awamu tatu za mwanzo za operesheni hiyo zilisababisha kukamatwa kwa raia 151 wa Misri na wageni 540, huku silaha, magari na vifaa mbalimbali vikikamatwa.
Jeshi la Misri limeeleza kuwa halitasitisha juhudi zake za kukabiliana na makundi yanayohusika na shughuli hizo, likisisitiza umuhimu wa kulinda mipaka, usalama wa taifa na utajiri wa asili wa nchi hiyo.

Aidha, limetangaza maandalizi ya kuanza awamu ya nne ya operesheni dhidi ya uchimbaji haramu wa dhahabu kuanzia Novemba 7, 2026.
Hata hivyo, taarifa zilizotolewa kuhusu vifo vya maafisa hao hazijaweka wazi idadi ya watu waliokuwa upande wa makundi yaliyokabiliana na jeshi waliofariki au kujeruhiwa katika mapambano hayo.

Post a Comment