Trump Atuma Ujumbe Huu Wa Ghafla Uganda Amtaja Bobi wine

WASHINGTON D.C. – Mwenyekiti wa Kamati ya Masuala ya Kigeni katika Seneti ya Marekani, Jim Risch, ameitaka Wizara ya Mambo ya Nje ya nchi hiyo kufanya tathmini ya kina kuhusu uhusiano wa kidiplomasia kati ya Marekani na Uganda.

Hatua hiyo imekuja kufuatia mivutano ya kisiasa inayozidi kufukuta nchini Uganda mara baada ya kumalizika kwa uchaguzi mkuu uliomrejesha madarakani Rais Yoweri Kaguta Museveni.

Mbali na kauli ya Seneta Risch, aliyekuwa Rais wa Marekani, Donald Trump, ametoa onyo kali akibainisha kuwa anafuatilia kwa ukaribu yanayoendelea nchini humo. 

Katika kauli yake, Trump amesisitiza kuwa hatapendelea kuona usalama wa kiongozi wa upinzani, Robert Kyagulanyi, maarufu kama Bobi Wine, ukiingiliwa.

Uchaguzi huo mkuu ulimtangaza Rais Museveni kuwa mshindi kwa kura takribani 71%, ushindi unaompa nafasi ya kuongoza taifa hilo kwa muhula wa saba.

Hata hivyo, matokeo hayo yamepingwa vikali na Bobi Wine, kiongozi wa chama cha National Unity Platform (NUP), aliyeshika nafasi ya pili kwa kupata asilimia 20 ya kura zote. 

Bobi Wine amedai kuwa mchakato huo uligubikwa na ukosefu wa haki na ukiukwaji wa misingi ya kidemokrasia.

Tathmini inayopendekezwa na Seneta Risch inaweza kuwa na athari kubwa kwa Uganda, ikizingatiwa kuwa Marekani ni mshirika mkubwa wa nchi hiyo katika masuala ya:

Misaada ya kijeshi na usalama.

Miradi ya afya na maendeleo ya jamii.

Ushirikiano wa kibiashara na kikanda.

Hadi sasa, Serikali ya Uganda haijatoa tamko rasmi kufuatia shinikizo hilo jipya kutoka kwa viongozi wa juu wa Marekani.

Post a Comment

Previous Post Next Post