Licha ya kauli za ushindi kutoka kwa Rais wa Marekani Donald Trump, wachambuzi wa siasa za kimataifa wanasema vita dhidi ya Iran bado havijafikia hatua ambayo Washington inaweza kutangaza ushindi.
Baada ya karibu wiki mbili za mapigano kati ya Marekani, Israel na Iran, hali inaonyesha kuwa mgogoro huo unaendelea kuwa mgumu kisiasa, kijeshi na kiuchumi.
Hapa kuna sababu kadhaa zinazoonyesha kwanini ushindi wa haraka bado haujaonekana.
Kwanza ni kufungwa kwa njia muhimu ya mafuta duniani ya Strait of Hormuz. Iran imezuia sehemu ya njia hiyo ambayo hupitisha takribani asilimia 20 ya mafuta ya dunia.
Wataalamu wa usalama wanasema kufungua njia hiyo kwa nguvu ni kazi ngumu kwa sababu Iran inaweza kutumia ndege ndogo zisizo na rubani na makombora ya gharama ndogo kuzuia meli kupita.
Sababu ya pili ni uongozi mpya wa Iran. Baada ya kuuawa kwa kiongozi wa zamani Ali Khamenei katika mashambulizi ya mwanzo ya vita, nafasi yake ilichukuliwa na mwanawe Mojtaba Khamenei.
Baada ya karibu wiki mbili za mapigano kati ya Marekani, Israel na Iran, hali inaonyesha kuwa mgogoro huo unaendelea kuwa mgumu kisiasa, kijeshi na kiuchumi.
Hapa kuna sababu kadhaa zinazoonyesha kwanini ushindi wa haraka bado haujaonekana.
Kwanza ni kufungwa kwa njia muhimu ya mafuta duniani ya Strait of Hormuz. Iran imezuia sehemu ya njia hiyo ambayo hupitisha takribani asilimia 20 ya mafuta ya dunia.
Hatua hiyo imeongeza bei ya mafuta duniani na kuleta changamoto kubwa kwa jeshi la majini la Marekani ambalo lingeingia katika hatari kubwa kujaribu kufungua njia hiyo kwa nguvu za kijeshi.
Sababu ya pili ni uongozi mpya wa Iran. Baada ya kuuawa kwa kiongozi wa zamani Ali Khamenei katika mashambulizi ya mwanzo ya vita, nafasi yake ilichukuliwa na mwanawe Mojtaba Khamenei.
Hali hiyo imeonyesha kuwa serikali ya Iran haikuanguka kama ilivyotarajiwa na baadhi ya viongozi wa Marekani.
Sababu ya tatu ni tofauti za kimkakati kati ya Marekani na Israel. Ingawa mataifa hayo mawili yanashirikiana katika mashambulizi dhidi ya Iran, wachambuzi wanaona kuwa malengo yao ya mwisho yanaweza kutofautiana.

Israel inaonekana kuwa tayari kuendelea na mapigano kwa muda mrefu zaidi ili kuhakikisha usalama wake wa kikanda.
Sababu nyingine ni ukosefu wa mkakati wazi wa kumaliza vita. Kauli za viongozi wa Marekani zimekuwa zikibadilika kuhusu malengo ya vita, jambo linalofanya iwe vigumu kuunda simulizi moja la ushindi.
Pia kuna swali kuhusu mpango wa nyuklia wa Iran. Ingawa Marekani inasema imeharibu miundombinu mingi ya kijeshi, wataalamu wanaamini Iran bado inaweza kuwa na akiba ya uranium iliyoongezwa nguvu ambayo inaweza kuruhusu nchi hiyo kuanzisha tena mpango wake wa nyuklia siku zijazo.
Changamoto nyingine ni hali ya kisiasa ndani ya Iran. Mwanzoni mwa vita, Trump alitoa wito kwa wananchi wa Iran kuasi dhidi ya serikali yao.

Hata hivyo hadi sasa hakuna ishara kubwa ya maandamano ya kitaifa dhidi ya utawala wa Tehran.
Hatimaye kuna shinikizo la kisiasa ndani ya Marekani. Kupanda kwa bei ya mafuta na gharama za vita kunaweza kuathiri uchumi wa raia wa kawaida.

Kadri muda unavyopita na hasara za kijeshi kuongezeka, wapiga kura wanaweza kuanza kuhoji faida ya vita hivyo.
Wachambuzi wanasema vita vingi vya kisasa havimaliziki kwa ushindi wazi kama ilivyotokea katika Vita Kuu ya Pili ya Dunia.

Badala yake mara nyingi huisha kupitia mazungumzo ya kisiasa au makubaliano ya muda.
Kwa sasa, mgogoro kati ya Marekani na Iran unaendelea huku dunia ikifuatilia kwa karibu kama vita hivyo vitaongezeka au kufikia suluhisho la kidiplomasia.

Post a Comment