Rais wa zamani wa Marekani, Donald J. Trump, amezua mjadala mkubwa kimataifa baada ya kudai kuwa Marekani imefanya moja ya mashambulizi makubwa zaidi ya mabomu katika historia ya Mashariki ya Kati.
Hata hivyo, Trump alisisitiza kuwa licha ya uwezo mkubwa wa silaha za Marekani, hakutoa amri ya kushambulia miundombinu ya mafuta ya kisiwa hicho.
Kupitia ujumbe uliosambaa mitandaoni, Trump alisema kuwa mashambulizi hayo yalifanywa kwa maelekezo yake na kutekelezwa na Jeshi la Marekani kupitia Kamandi Kuu ya Marekani (CENTCOM), yakilenga malengo ya kijeshi katika Kisiwa cha Kharg nchini Iran.
Katika ujumbe huo, Trump alidai kuwa mashambulizi hayo “yameharibu kabisa kila shabaha ya kijeshi” katika kisiwa hicho ambacho mara nyingi hutajwa kuwa moja ya maeneo muhimu kwa Iran.
Kisiwa cha Kharg Island kinajulikana sana kwa umuhimu wake katika usafirishaji wa mafuta ya Iran, na ni kitovu kikubwa cha miundombinu ya mafuta inayounganisha Iran na soko la kimataifa.
Alisema alichukua uamuzi huo kwa “sababu za heshima na maadili,” akiongeza kuwa uharibifu wa miundombinu hiyo ungeweza kuathiri vibaya soko la mafuta duniani na kuongeza mvutano wa kimataifa.
Katika kauli yake, Trump pia alitoa onyo kali kwa Iran akisema kuwa iwapo taifa hilo au washirika wake watajaribu kuzuia uhuru wa usafiri wa meli katika Mlango wa Bahari wa Strait of Hormuz, Marekani inaweza kufikiria upya uamuzi wa kutoiharibu miundombinu ya mafuta ya kisiwa hicho. Mlango huo wa bahari ni mojawapo ya njia muhimu zaidi za biashara ya mafuta duniani, ambapo sehemu kubwa ya mafuta ya Mashariki ya Kati hupitia katika njia hiyo.
Trump alisisitiza kuwa Jeshi la Marekani ni moja ya majeshi yenye nguvu zaidi duniani, akidai kuwa Iran haina uwezo wa kulinda chochote ambacho Marekani itaamua kushambulia.

Aidha, alirudia msimamo wake mkali kuhusu silaha za nyuklia akisema kuwa Iran haitaruhusiwa kamwe kumiliki silaha za nyuklia au kutishia Marekani, Mashariki ya Kati au dunia kwa ujumla.
Kauli hiyo imeibua mjadala mkubwa katika siasa za kimataifa, huku wachambuzi wakisema kuwa taarifa kama hizo zinaweza kuongeza mvutano katika eneo la Mashariki ya Kati.
Kauli hiyo imeibua mjadala mkubwa katika siasa za kimataifa, huku wachambuzi wakisema kuwa taarifa kama hizo zinaweza kuongeza mvutano katika eneo la Mashariki ya Kati.
Baadhi ya wachambuzi wanaonya kuwa matamshi makali kati ya Marekani na Iran yanaweza kuongeza hatari ya migogoro ya kijeshi katika eneo hilo.
Hadi sasa, mamlaka za Iran hazijatoa tamko rasmi kuthibitisha au kukanusha madai hayo. Hata hivyo, tukio hilo linaendelea kufuatiliwa kwa karibu na jumuiya ya kimataifa huku dunia ikisubiri kuona iwapo mvutano huo utaendelea kuongezeka au utapata suluhisho la kidiplomasia.

Post a Comment