Iran Yatoa Onyo Kali kwa Marekani! Yasema Kambi Zake za Kijeshi Mashariki ya Kati Sio Salama Tena


Tafadhali Zingatia: Ikiwa unasoma kwenye PHOENIX, tafadhali bofya kitufe cha “Soma Makala Asili” kilicho upande wa juu kulia ili kusoma makala kamili.

TEHRAN – Iran imeongeza joto la mvutano wa kidiplomasia na kijeshi baada ya kutoa onyo kali ikisema kuwa kambi za kijeshi za Marekani zilizopo katika eneo la Mashariki ya Kati hazitachukuliwa tena kama maeneo salama, zikielezwa kuwa zinachangia kuleta hali ya kutokuwa na utulivu katika ukanda huo.

Kwa mujibu wa taarifa za Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (Islamic Revolutionary Guard Corps), vikosi vya Iran vimefanikiwa kuzuia kile walichokiita jaribio la uvamizi wa ardhini katika maeneo ya mipaka ya nchi hiyo, sambamba na kudai kuangusha ndege isiyo na rubani (droni) inayodaiwa kuwa ya Marekani wakati wa mivutano inayoendelea kati ya mataifa hayo mawili.


Post a Comment

Previous Post Next Post