Mbunge wa CCM Afunguka Mazito Kuhusu Muungano, Asema Tatizo Siyo Bara

Mbunge wa Geita, Joseph Kasheku Musukuma, ametoa maoni yake kuhusu mjadala wa Muungano wa Tanzania, akisema baadhi ya viongozi na wabunge kutoka Zanzibar hutumia hoja za Muungano kuficha changamoto za maendeleo katika maeneo yao.

Akizungumza katika mahojiano kupitia M&S Podcast, Musukuma alisema Muungano umejikita kwa muda mrefu katika maisha ya Watanzania kiasi kwamba vizazi vya sasa vimechanganyika kupitia ndoa, biashara na shughuli mbalimbali za kijamii. Kwa mtazamo wake, hali hiyo imeufanya Muungano kuwa sehemu ya maisha ya wananchi na si jambo rahisi kutenganishwa.

Musukuma alidai kuwa baadhi ya viongozi kutoka Zanzibar wanaposhindwa kutatua changamoto zinazowakabili wananchi wao, huelekeza lawama kwa Muungano badala ya kutafuta suluhisho la matatizo hayo. Amesema viongozi wanapaswa kuelekeza nguvu katika kutekeleza wajibu wao wa kuwaletea wananchi maendeleo badala ya kuendeleza mijadala inayogawanya maoni.......BONYEZA HAPA USOMA TAARIFA YOTE.

Post a Comment

Previous Post Next Post