Wizara ya Ulinzi ya Saudi Arabia imethibitisha kuwa Ubalozi wa Marekani mjini Riyadh ulishambuliwa kwa ndege mbili zisizo na rubani mnamo Jumatatu, Machi 2, 2026.
Ripoti za awali kutoka vyombo vya habari vya kimataifa zimetofautiana kuhusu athari za shambulio hilo.
Tukio hilo lilisababisha moto na uharibifu wa vifaa katika jengo la ubalozi, huku uchunguzi ukiendelea kubaini chanzo na wahusika wa shambulio hilo.
wa mujibu wa taarifa iliyotolewa kupitia mtandao wa X, moto uliosababishwa na shambulio hilo ulidhibitiwa na vikosi vya usalama, ingawa picha za awali zilionyesha moshi mzito ukipaa juu ya eneo la ubalozi.
Wizara ya Ulinzi ya Saudi Arabia imeeleza kuwa hatua za kiusalama zimeimarishwa katika miji ya Riyadh, Jeddah na Dhahran, ambapo wafanyakazi wa ubalozi wameelekezwa kusalia majumbani mwao kwa tahadhari.
Ripoti za awali kutoka vyombo vya habari vya kimataifa zimetofautiana kuhusu athari za shambulio hilo.
Wakati Saudi Arabia ikieleza kuwa uharibifu ni mdogo na hakuna majeruhi waliothibitishwa rasmi, taarifa zisizo rasmi zimeeleza kuwa wanajeshi sita wa Marekani wamepoteza maisha na wengine 18 kujeruhiwa. Hata hivyo, idadi hiyo haijathibitishwa na vyanzo vya kuaminika, na bado inachunguzwa.
Tukio hili limeibua hofu ya kuongezeka kwa mvutano wa kikanda, hasa ikizingatiwa kuwa linatokea katika kipindi ambacho Iran imekuwa ikitoa vitisho vya kulipiza kisasi kufuatia mashambulizi ya Marekani na Israel dhidi ya Tehran na Beirut.

Wachambuzi wa usalama wa kimataifa wanaonya kuwa shambulio hili linaweza kuwa ishara ya kuongezeka kwa mashambulizi ya kulipiza kisasi dhidi ya maslahi ya Marekani na washirika wake katika Mashariki ya Kati.
Kwa sasa, hali ya tahadhari imeendelea kuimarishwa, huku uchunguzi wa pamoja ukifanywa na Saudi Arabia na Marekani ili kubaini wahusika na malengo ya shambulio hilo.
Kwa sasa, hali ya tahadhari imeendelea kuimarishwa, huku uchunguzi wa pamoja ukifanywa na Saudi Arabia na Marekani ili kubaini wahusika na malengo ya shambulio hilo.
Tukio hili linaibua maswali mapya kuhusu usalama wa balozi za kigeni katika eneo hilo, na linaweza kuathiri uhusiano wa kidiplomasia kati ya Riyadh na Washington.
Post a Comment