Mvutano mkubwa kati ya Iran na Marekani umeendelea kuongezeka baada ya Iran kutekeleza mashambulizi dhidi ya kambi ya kijeshi ya Marekani mapema Alhamisi, hatua ambayo Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran (IRGC) limesema ilikuwa ni jibu la moja kwa moja kwa mashambulizi ya Marekani karibu na Bandar Abbas.
Kwa mujibu wa taarifa zilizoripotiwa na Reuters, IRGC ilisema kuwa shambulio hilo lilifanyika baada ya vikosi vya Marekani kushambulia kituo cha kudhibiti ndege zisizo na rubani kusini mwa Iran na kukiharibu.
Ingawa IRGC haikutaja rasmi eneo lililolengwa katika mashambulizi yake, ripoti kadhaa zilieleza kuwa makombora na ndege zisizo na rubani zilielekezwa nchini Kuwait, ambako Marekani ina vituo vya kijeshi.

Vyombo vya habari vya Iran vilieleza tukio hilo kama “shambulio la kulipiza kisasi” dhidi ya kile Tehran ilichokiita ukiukwaji wa makubaliano ya kusitisha mapigano pamoja na uchokozi wa Marekani katika eneo la Strait of Hormuz.
Marekani kwa upande wake ilisema mashambulizi yake yalikuwa ya kujilinda baada ya kudai kuwa ndege nne zisizo na rubani kutoka Iran zilikuwa zikisogea karibu na meli zake katika eneo hilo.

Marekani ilieleza kuwa ilizitungua ndege hizo kabla ya kushambulia kituo cha ardhini kilichokuwa kikijiandaa kurusha ndege nyingine ya tano.
Ingawa IRGC haikutaja rasmi eneo lililolengwa katika mashambulizi yake, ripoti kadhaa zilieleza kuwa makombora na ndege zisizo na rubani zilielekezwa nchini Kuwait, ambako Marekani ina vituo vya kijeshi.
Serikali ya Kuwait ilithibitisha kuwa mifumo yake ya ulinzi wa anga ilifanikiwa kukabiliana na vitisho hivyo bila kuripotiwa kwa madhara makubwa au vifo.
Katika taarifa yake, IRGC ilionya kuwa uchokozi wowote mwingine kutoka Marekani utakabiliwa na “majibu mabaya na ya kutisha,” ikisisitiza kuwa Iran haitakubali mashambulizi dhidi ya ardhi yake au vikosi vyake vya kijeshi.

Kauli hiyo imeongeza hofu kuhusu mustakabali wa makubaliano dhaifu ya kusitisha mapigano pamoja na mazungumzo ya amani yanayoendelea kupitia Qatar na Oman.
Wachambuzi wa siasa za kimataifa wanaeleza kuwa hali hiyo inaweza kuathiri kwa kiasi kikubwa juhudi za kidiplomasia zilizokuwa zikilenga kufungua tena biashara kupitia Strait of Hormuz pamoja na kujadili mustakabali wa mpango wa nyuklia wa Iran.

Njia hiyo ya baharini ni muhimu sana kwa uchumi wa dunia kwa sababu sehemu kubwa ya mafuta ya kimataifa hupitia eneo hilo kila siku.
Mvutano huo pia umeongeza hofu ya kuzuka kwa vita kubwa zaidi katika eneo la Ghuba ya Uajemi, jambo ambalo linaweza kuathiri biashara ya kimataifa, usafirishaji wa mafuta na usalama wa mataifa mengi duniani.

Mataifa mbalimbali yameendelea kutoa wito kwa Marekani na Iran kutumia mazungumzo ya kidiplomasia badala ya kuongeza mashambulizi ya kijeshi.
Kwa sasa dunia inaendelea kufuatilia kwa karibu hatua zinazochukuliwa na Washington pamoja na Tehran huku kukiwa na hofu kwamba hali hiyo inaweza kuingia katika awamu mpya ya mapigano ikiwa juhudi za mazungumzo hazitafanikiwa kwa wakati.
TAZAMA VIDEO.

Post a Comment