Mvutano kati ya Marekani na Iran umeendelea kuongezeka baada ya serikali ya Tehran kuishutumu Washington kwa kufanya mashambulizi mapya karibu na mji wa Bandar Abbas kusini mwa Iran, hatua ambayo Iran imeitaja kuwa ni ukiukwaji mkubwa wa sheria za kimataifa na makubaliano ya usitishaji mapigano.
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran, Esmaeil Baghaei, alisema mashambulizi hayo yaliyotekelezwa alfajiri ya Alhamisi yalikiuka Mkataba wa Umoja wa Mataifa pamoja na uhuru wa taifa la Iran.
Hata hivyo, Iran imekanusha hoja hizo na kusema Marekani imekuwa ikikiuka makubaliano ya usitishaji mapigano mara kwa mara tangu yalipoanza kutekelezwa Aprili 8.

Serikali ya Iran pia imeutaka Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuchukua hatua dhidi ya Marekani kwa kile ilichokiita uchokozi dhidi ya mipaka na mamlaka ya Iran.
Kwa mujibu wa taarifa mbalimbali, mashambulizi hayo yalitokea karibu na Bandar Abbas, eneo muhimu karibu na Mlango wa Bahari wa Hormuz ambao ni njia nyeti ya usafirishaji wa mafuta duniani.

Marekani kupitia CENTCOM ilisema kuwa ilifanya mashambulizi hayo kwa lengo la kujilinda baada ya kudai kuwa Iran ilikuwa ikiandaa mashambulizi ya kutumia ndege zisizo na rubani katika eneo hilo.
Ripoti zinaonyesha kuwa majeshi ya Marekani yalidungua ndege nne zisizo na rubani za Iran karibu na Strait of Hormuz kabla ya kushambulia kituo cha ardhini kilichodaiwa kuwa kinaandaa kuzindua drone nyingine.

Marekani imeeleza kuwa hatua hizo zilikuwa za “kujilinda” na zililenga kudumisha usitishaji mapigano uliopo.
Hata hivyo, Iran imekanusha hoja hizo na kusema Marekani imekuwa ikikiuka makubaliano ya usitishaji mapigano mara kwa mara tangu yalipoanza kutekelezwa Aprili 8.
Tehran pia imeishutumu Washington kwa kufanya mashambulizi dhidi ya meli za biashara katika Ghuba ya Uajemi na kuongeza vitisho dhidi ya mataifa ya eneo hilo.
Katika hatua ya kulipiza kisasi, Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran (IRGC) lilitangaza kuwa lililenga kambi ya kijeshi ya Marekani katika eneo la Ghuba.

Baadhi ya ripoti zilisema kuwa makombora yalielekezwa kuelekea Kuwait kabla ya kuzuiwa na mifumo ya ulinzi wa anga ya taifa hilo.
Wachambuzi wa siasa za kimataifa wanaeleza kuwa hali hiyo inaonyesha namna usitishaji mapigano kati ya Iran na Marekani ulivyo dhaifu.

Licha ya mazungumzo ya kidiplomasia yanayoendelea kuhusu mpango wa nyuklia wa Iran na usalama wa Strait of Hormuz, mashambulizi ya kijeshi yanaendelea kuongeza hofu ya kurejea kwa vita vikubwa katika Mashariki ya Kati.
Aidha, Iran imeonyesha mshikamano wake na Oman baada ya matamshi ya viongozi wa Marekani yaliyotafsiriwa kama vitisho dhidi ya taifa hilo.

Tehran imesema Oman imekuwa na mchango mkubwa katika juhudi za amani na upatanishi katika eneo la Mashariki ya Kati.
Kwa sasa, dunia inaendelea kufuatilia kwa karibu mvutano huu huku mataifa mengi yakihofia athari kubwa za kiuchumi na kisiasa iwapo hali itazidi kuwa mbaya.

Wataalamu wa usalama wanaonya kuwa kuendelea kwa mashambulizi na vitisho kunaweza kuhatarisha biashara ya mafuta duniani pamoja na utulivu wa eneo lote la Ghuba ya Uajemi.
TAZAMA VIDEO.
TAZAMA VIDEO.
Post a Comment