Mvutano kati ya Marekani na Iran umeendelea kuongezeka baada ya Waziri wa Hazina wa Marekani, Scott Bessent, kutangaza hatua mpya kali dhidi ya Iran pamoja na onyo kali kwa Oman kuhusu suala la ushuru katika Mlango wa Hormuz.
Mlango wa Hormuz ni moja ya njia muhimu zaidi duniani kwa usafirishaji wa mafuta na gesi. Sehemu kubwa ya mafuta ya dunia hupitia katika eneo hilo kuelekea Asia, Ulaya na mataifa mengine.
Kauli hiyo imeongeza mjadala mkubwa wa kimataifa kuhusu usalama wa biashara ya mafuta, usafiri wa anga pamoja na hali ya kisiasa katika Mashariki ya Kati.
Kupitia ujumbe aliouchapisha kwenye mtandao wa kijamii wa X, Bessent alisema Marekani itachukua hatua za kuzuia ndege za Iran kupata huduma muhimu za kimataifa.

Alisema Marekani itafunga fursa za ndege za Iran kutua katika viwanja mbalimbali vya ndege, kupata mafuta ya ndege pamoja na kufanya mauzo ya tiketi katika maeneo mengi duniani.
Hata hivyo, Bessent alifafanua kuwa Marekani haitazuia safari za kidini au misaada ya kibinadamu. Alisema Wairan wanaotaka kwenda hija katika miji mitakatifu ya Makka na Madina wataruhusiwa kusafiri, pamoja na watu wenye sababu za kibinadamu zinazokubalika kimataifa.
Kauli hiyo ilikuja muda mfupi baada ya Marekani kuweka vikwazo dhidi ya taasisi mpya ya Iran inayojulikana kama Persian Gulf Strait Authority, ambayo Tehran imeianzisha kwa ajili ya kusimamia shughuli za meli zinazopita katika Mlango wa Hormuz.

Serikali ya Marekani inaamini kuwa taasisi hiyo inalenga kukusanya ushuru kutoka kwa meli zinazopita katika njia hiyo muhimu ya bahari.
Mlango wa Hormuz ni moja ya njia muhimu zaidi duniani kwa usafirishaji wa mafuta na gesi. Sehemu kubwa ya mafuta ya dunia hupitia katika eneo hilo kuelekea Asia, Ulaya na mataifa mengine.
Kutokana na umuhimu wake mkubwa, mvutano wowote katika eneo hilo mara nyingi husababisha hofu ya kupanda kwa bei ya mafuta pamoja na kuyumba kwa uchumi wa dunia.
Bessent pia aliionya Oman, akisema Marekani haitakubali taifa lolote kusaidia Iran kuanzisha mfumo wa ushuru katika Mlango wa Hormuz.

Alisema Wizara ya Hazina ya Marekani iko tayari kuwawekea vikwazo watu binafsi, taasisi za kifedha au washirika wowote watakaosaidia mpango huo moja kwa moja au kwa njia isiyo ya moja kwa moja.
Kwa mujibu wa Bessent, alizungumza na balozi wa Oman mjini Washington na kupata uhakikisho kwamba Oman haina mpango wa kushiriki katika utozaji wa ushuru kwa meli zinazopita katika Mlango wa Hormuz.

Alisema aliweka wazi kuwa Marekani haitakubali hatua yoyote inayoweza kuathiri uhuru wa biashara ya kimataifa katika njia hiyo muhimu.
Mvutano huu umeongezeka tangu kuanza kwa vita kati ya Marekani, Israel na Iran mwishoni mwa mwezi Februari, ambapo shughuli za biashara katika Mlango wa Hormuz zimeathirika kwa kiwango kikubwa.

Ripoti mbalimbali zinaonyesha kuwa gharama za nishati zimeendelea kupanda duniani kutokana na hofu ya kuvurugika kwa usafirishaji wa mafuta.
Wakati huo huo, Marekani na Iran zimeendelea kuwa katika hali ya kusitisha mapigano tangu Aprili 8 huku mazungumzo ya kidiplomasia yakiendelea kupitia wapatanishi wa kimataifa akiwemo Pakistan.

Hata hivyo, mashambulizi na vitisho kati ya pande hizo bado vinaendelea kuripotiwa mara kwa mara.
Wachambuzi wa siasa za kimataifa wanaonya kuwa kuongezeka kwa vikwazo, vitisho vya kiuchumi pamoja na mvutano wa kijeshi kunaweza kuongeza hatari ya mgogoro mkubwa zaidi katika Mashariki ya Kati.

Mataifa mbalimbali duniani yanaendelea kutoa wito wa mazungumzo ya amani ili kuzuia hali hiyo isiathiri zaidi uchumi wa dunia na usalama wa kimataifa.
TAZAMA VIDEO.
TAZAMA VIDEO.
Post a Comment