Aoa Mwanaume Mwenzie Akidhania Ni Mwanamke Siri Yagundulika Baada Ya Mwaka Mmoja

Kijana mmoja mwenye umri wa miaka 26 nchini Indonesia amekuwa gumzo kubwa mitandaoni baada ya kudaiwa kugundua kuwa mtu aliyekuwa amemuoa kama mke wake alikuwa ameficha utambulisho wake wa kweli kwa muda mrefu, jambo lililosababisha mshtuko mkubwa kwa familia na jamii iliyokuwa karibu na wanandoa hao.

Kwa mujibu wa taarifa zilizosambaa katika vyombo mbalimbali vya habari na mitandao ya kijamii, kijana huyo alikuwa katika mahusiano ya kimapenzi kwa takribani mwaka mmoja kabla ya kufikia uamuzi wa kufunga ndoa. 

Katika kipindi hicho chote, aliamini kuwa alikuwa katika uhusiano wa kawaida na mwanamke ambaye alimtaja kuwa mwenye tabia njema, heshima na maadili yaliyomvutia kuamua kumuoa.

Inaelezwa kuwa katika muda wote wa uchumba, mwenza huyo alikuwa akivaa hijabu pamoja na mavazi yaliyofunika sehemu kubwa ya mwili wake. 

Kutokana na hali hiyo, baadhi ya watu wanaamini kuwa ilikuwa vigumu kwa kijana huyo kugundua ukweli kuhusu utambulisho wa mwenzake mapema.

Taarifa zinaeleza kuwa baada ya kufunga ndoa, mambo yalianza kuzua maswali kadhaa ndani ya familia. Baadhi ya ndugu walidai waliona mienendo isiyo ya kawaida ambayo iliwafanya waanze kuwa na mashaka kuhusu utambulisho wa mmoja wa wanandoa hao.

Post a Comment

Previous Post Next Post