Rais wa Marekani, Donald Trump, ameionya Iran kuwa itakabiliwa na mashambulizi mengine makubwa ya kijeshi iwapo haitasitisha kile alichodai kuwa ni uungaji mkono wake kwa vikundi washirika vinavyofanya shughuli nchini Lebanon.[Tazama video].
Trump amesema kuwa utawala wa Tehran unapaswa kusitisha mara moja msaada wake kwa makundi hayo, akisisitiza kuwa Marekani iko tayari kuchukua hatua kali zaidi za kijeshi endapo Iran itaendelea na kile ilichokiita vitendo vya kuhatarisha usalama wa eneo la Mashariki ya Kati.
Kauli hiyo imeongeza mvutano kati ya mataifa hayo mawili, huku ikionyesha msimamo mkali wa Washington kuhusu ushawishi wa Iran katika eneo hilo.
Serikali ya Marekani imekuwa ikiishutumu Iran kwa muda mrefu kwa kuunga mkono makundi yenye silaha yanayofanya shughuli katika nchi mbalimbali za Mashariki ya Kati, madai ambayo Tehran imekuwa ikiyakanusha mara kwa mara.
Tamko la Trump limetolewa wakati ujumbe wa ngazi ya juu wa Iran, ukiongozwa na Mohammad Bagher Ghalibaf, ukiendelea na mazungumzo na ujumbe wa Marekani unaoongozwa na Makamu wa Rais JD Vance.
Tamko la Trump limetolewa wakati ujumbe wa ngazi ya juu wa Iran, ukiongozwa na Mohammad Bagher Ghalibaf, ukiendelea na mazungumzo na ujumbe wa Marekani unaoongozwa na Makamu wa Rais JD Vance.
Mazungumzo hayo yanatajwa kulenga kujadili masuala ya usalama wa kikanda pamoja na kupunguza mvutano unaoendelea kati ya pande hizo mbili.
Wachambuzi wa siasa za kimataifa wanaeleza kuwa kauli ya Trump inaweza kuongeza shinikizo kwa Iran katika mazungumzo hayo, huku dunia ikiendelea kufuatilia kwa karibu hatua zitakazochukuliwa na pande zote katika siku zijazo.

Post a Comment