Watoto wa viongozi wakuu wa nchi mara nyingi hujikuta wakivuta hisia za wananchi wanapoamua kuingia kwenye siasa au kushika nafasi mbalimbali za uongozi wa umma.
Tanzania nayo imekuwa na mifano kadhaa ya watoto wa marais waliowahi kushika au wanaoendelea kushika nafasi muhimu katika uongozi wa kisiasa na serikali.
Wapo waliochaguliwa na wananchi kupitia uchaguzi, walioteuliwa katika nafasi za serikali, pamoja na waliopata nafasi za uwakilishi kupitia vyama vyao vya siasa.
Miongoni mwao ni Dkt. Hussein Ali Mwinyi, mtoto wa Rais wa Awamu ya Pili wa Tanzania, Ali Hassan Mwinyi. Dkt. Mwinyi alianza kujenga historia yake ya kisiasa kwa kuwa Mbunge wa Kwahani Zanzibar, kabla ya kuhudumu katika nafasi mbalimbali za uwaziri ndani ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mwaka 2020 alichaguliwa kuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, nafasi ambayo anaendelea kuitumikia hadi sasa. Uongozi wake umejikita katika kuimarisha uchumi wa Zanzibar, uwekezaji na utoaji wa huduma za kijamii.SOMA ZAIDI.
Post a Comment