Mjadala Mkali Wazuka Baada ya Mwigulu Kupendekeza Jina Jipya kwa Kuku wa Dodoma na Singida

Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba, amependekeza kuku wanaofugwa katika mikoa ya Dodoma na Singida watambulike kwa jina la Kuku wa Kanda ya Kati, badala ya kuendelea kuitwa kuku wa kienyeji, akisema mabadiliko hayo yataongeza utambulisho na thamani ya bidhaa hiyo katika soko la ndani na nje ya nchi.

Akizungumza Agosti 1, 2026 wakati wa ufunguzi wa Maonesho ya Kilimo ya Nanenane yaliyofanyika katika Viwanja vya Dkt. John Malecela jijini Dodoma, Dkt. Mwigulu alisema kuku hao wamekuwa alama ya uzalishaji wa Kanda ya Kati na wanapaswa kutambulishwa kwa jina linaloakisi eneo wanakotoka.

Amesema bidhaa nyingi za kilimo nchini zimejijengea soko kutokana na kutambulishwa kwa majina ya maeneo zinakozalishwa, jambo ambalo limeongeza ubora na ushindani wake. Kwa mtazamo wake, utaratibu huo unapaswa kutumika pia kwa kuku wanaofugwa Dodoma na Singida.

“Tunapotaja mchele tunaambiwa ni wa Shinyanga au wa Kyela, na tukizungumzia ndizi tunaambiwa ni za Bukoba au Moshi. Lakini tukifika kwenye kuku wa Singida na Dodoma tunaambiwa ni kuku wa kienyeji. Hilo linapunguza utambulisho wao, hivyo waitwe Kuku wa Kanda ya Kati,” alisema Waziri Mkuu.

Post a Comment

Previous Post Next Post