Hatua ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kuhusisha jaji mwandamizi kutoka Namibia katika Tume ya Uchunguzi wa Makosa ya Jinai inayochunguza matukio yaliyojitokeza wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025, imezua mjadala mpana kuhusu sababu na umuhimu wa uamuzi huo.
Kilichoonekana wazi ni kwamba Serikali imelenga kuimarisha uaminifu, uwazi na hadhi ya kimataifa ya tume hiyo kwa kuhusisha mtaalamu wa mahakama kutoka nje ya Tanzania mwenye uzoefu wa muda mrefu katika mfumo wa haki.
Kwa mujibu wa taarifa rasmi iliyotolewa Agosti 5, 2026 na Tume ya Utumishi wa Mahakama ya Namibia (Judicial Service Commission - JSC), Jaji Mkuu wa Namibia, Peter S. Shivute, amemteua Naibu Jaji Mkuu wa nchi hiyo, Jaji Petrus T. Damaseb, kuwa mjumbe wa Tume hiyo kufuatia ombi rasmi kutoka Tanzania.
Post a Comment