Dkt.Ryoba Afichua Kuhusu Kigogo Huyu Aliyemshawishi Kuandika Barua Ya Kujiuzulu

Aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Dkt. Ayoub Ryoba, amefichua namna alivyofikia hatua ya kuandika barua ya kuachia nafasi hiyo baada ya kukabiliwa na mazingira aliyodai kuwa ya majungu, fitina na taarifa zisizo na uhalisia kuhusu utendaji wake.

Dkt. Ryoba ameeleza kuwa kipindi fulani akiwa katika uongozi wa TBC, alijikuta akikabiliwa na taarifa zilizowasilishwa kwa viongozi wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, hali iliyosababisha akemwe hadharani kabla viongozi hao hawajafika katika shirika hilo kujionea changamoto zilizokuwepo.

Akizungumza katika mahojiano na M/S Podcast yaliyorushwa Jumatano, Agosti 5, 2026, Dkt. Ryoba alisema alihisi baadhi ya watu walikuwa wakitumia majungu na fitina badala ya uwezo wao wa kazi ili kuwafikisha viongozi taarifa zinazoweza kuwaathiri wengine.

Post a Comment

Previous Post Next Post