Mbeya, Juni 2026 — Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Mbeya, imemhukumu adhabu ya kifo Barnaba Daud Mtewele baada ya kupatikana na hatia ya kuwaua Herieth Lupembe na mwanafunzi Ivon Tatizo katika tukio lililotokea Wilaya ya Chunya, Mkoa wa Mbeya, Machi 31, 2024.
Mbali na hukumu hiyo ya kifo, mahakama pia imemhukumu Barnaba kifungo cha miaka kumi gerezani kwa kosa la kumjeruhi mtoto wake, Daud Barnaba Mtewele, mwenye umri wa miaka saba wakati wa tukio hilo. Mtoto huyo alinusurika licha ya kupata majeraha makubwa katika shambulio hilo.
Hukumu hiyo ilisomwa na Joackim Charles Tiganga baada ya mahakama kupitia ushahidi uliowasilishwa na upande wa mashtaka pamoja na upande wa utetezi.

Katika uamuzi wake, jaji alieleza kuwa ushahidi uliotolewa ulitosha kuthibitisha bila shaka yoyote kuwa Barnaba ndiye aliyefanya makosa yaliyokuwa yakimkabili.SOMA ZAIDI.
Post a Comment