Mwanamke anayedaiwa kuwa mzaliwa wa Mbeya, Tanzania, amekamatwa nchini Marekani baada ya mwajiri wake kumtuhumu kushiriki mpango wa kumuuza mtoto akiwa pamoja na mumewe, katika kashfa inayodaiwa kufikia thamani ya dola milioni 76 za Marekani.
TAZAMA VIDEO HAPA.
Kwa mujibu wa taarifa zilizosambaa kwenye mitandao ya kijamii, mwajiri wa mwanamke huyo ndiye aliyetoa tuhuma hizo kwa mamlaka za uhamiaji na polisi, akidai kuwa kulikuwa na mpango wa siri uliokuwa ukihusisha biashara haramu ya watoto.
Taarifa hizo zinaeleza kuwa uchunguzi wa awali ulianza baada ya mwajiri huyo kubaini kile kilichoelezwa kama “tabia za kushuku” na mazungumzo yaliyodaiwa kuhusisha mpango huo. Hata hivyo, mamlaka za Marekani bado hazijatoa taarifa rasmi kuthibitisha undani wa tuhuma hizo wala kiwango cha ushiriki wa washukiwa.
Video Yaasambaa Mitandaoni
Baada ya kukamatwa kwake, video inayoaminika kuhusiana na tukio hilo ilisambaa kwa kasi katika mitandao ya kijamii, na kuibua mjadala mkubwa miongoni mwa watumiaji wa mtandao.
Wengi walionyesha mshangao na kutoamini, huku wengine wakitaka uchunguzi wa kina ufanyike kabla ya hitimisho lolote kutolewa kuhusu tuhuma hizo nzito. SOMA ZAIDI.

Post a Comment