Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imetoa ufafanuzi kuhusu hali ya kisheria ya Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu, kufuatia taarifa mbalimbali zinazoendelea kusambazwa ndani na nje ya nchi kuhusu mwenendo wa kesi zinazomkabili mwanasiasa huyo.
Katika maelezo yake rasmi, Serikali imeeleza kuwa si sahihi kumtaja Tundu Lissu kama "kiongozi wa upinzani aliyefungwa gerezani" kwa kuwa bado hajapatikana na hatia na hajahukumiwa na mahakama yoyote yenye mamlaka ya kutoa hukumu.
Kwa mujibu wa Serikali, Lissu kwa sasa ni mtuhumiwa anayekabiliwa na mashauri ya jinai ambayo bado yako katika hatua za usikilizwaji mbele ya mahakama.
Ufafanuzi huo umetolewa kufuatia rasimu ya hoja iliyowasilishwa na baadhi ya wadau wa kimataifa waliotoa maoni kuhusu mwenendo wa kesi zinazomhusu kiongozi huyo wa upinzani.
Serikali imeeleza kuwa matumizi ya maneno yanayoashiria kuwa mtu tayari amehukumiwa yanaweza kupotosha ukweli wa kisheria na kuathiri uelewa wa umma kuhusu hatua halisi ya mashauri yaliyopo mahakamani.S.O.M.A Z.A.ID.I.
Post a Comment