Tafadhali Zingatia: Ikiwa unasoma kwenye PHOENIX, tafadhali bofya kitufe cha “Soma Makala Asili” kilicho upande wa juu kulia ili kusoma makala kamili.
WASHINGTON / TEHRAN — Rais wa Marekani, Donald Trump, ametangaza kuwa jeshi la Marekani limefanya mashambulizi ya anga dhidi ya maeneo kadhaa ya kijeshi ya Iran, katika hatua inayozidi kuongeza mvutano kati ya Washington na Tehran.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, mashambulizi yamelenga maghala ya makombora, vituo vya rada pamoja na ndege zisizo na rubani (drones) za Iran, hatua ambayo Marekani inasema ni jibu kwa kile inachokiita ukiukaji wa mara kwa mara wa makubaliano ya kusitisha mapigano.
Akizungumza kuhusu operesheni hiyo, Trump alitoa onyo kali akisema kuwa ikiwa Marekani itaendelea kulazimika kufanya mashambulizi zaidi, Iran inaweza kukabiliwa na hatari ya kutoweka kabisa.
Kauli hiyo imeongeza hofu ya kuongezeka kwa mzozo wa kijeshi kati ya mataifa hayo mawili yenye nguvu duniani, huku wachambuzi wakisema hali inaweza kuathiri usalama wa kikanda na masoko ya kimataifa ya nishati.

Post a Comment