Apigwa Hadi Kufariki Dunia Akituhumiwa Ameiba Mapipa 3

Tafadhali Zingatia: Ikiwa unasoma kwenye PHOENIX, tafadhali bofya kitufe cha “Soma Makala Asili” kilicho upande wa juu kulia ili kusoma makala kamili.

Kijana mwenye umri wa miaka 25, Ally Rajabu, mkazi wa Kata ya Maji ya Chai, Wilaya ya Arumeru mkoani Arusha, amefariki dunia baada ya kudaiwa kupigwa sehemu mbalimbali za mwili wake kwa tuhuma za kuiba mapipa matatu chakavu yaliyokuwa yakitumiwa na fundi ujenzi katika eneo hilo.

Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na Balozi wa eneo hilo, Christopher Ayo, akizungumza na GADI TV, tukio hilo lilitokea usiku wa kuamkia Juni 25, 2026. Inadaiwa kuwa Ally alikamatwa akiwa amebeba moja ya mapipa hayo, akilielekeza mahali alipokuwa tayari amehifadhi mengine mawili, akidaiwa kuwa na lengo la kuyauza kama chuma chakavu.

Balozi huyo amesema kuwa fundi ujenzi aliyekuwa akimiliki mapipa hayo alipobaini tukio hilo, alishirikiana na mtu mwingine kumkamata kijana huyo. Badala ya kumkabidhi mikononi mwa vyombo vya dola, inadaiwa walimshambulia kwa kumpiga sehemu mbalimbali za mwili wake, hali iliyosababisha apoteze maisha.

Tukio hilo limeibua hisia tofauti miongoni mwa wananchi wa eneo hilo, huku wengi wakikemea vitendo vya kujichukulia sheria mkononi na kusisitiza umuhimu wa kuwafikisha watuhumiwa wa uhalifu kwenye mamlaka husika ili hatua za kisheria zichukuliwe.Endelea Kusoma Kwa Kubofya Hapa.

Post a Comment

Previous Post Next Post