Mwanamke Ashikiliwa kwa Tuhuma za Kumuiba Mtoto Mchanga Hospitalini


Tafadhali Zingatia: Ikiwa unasoma kwenye PHOENIX, tafadhali bofya kitufe cha “Soma Makala Asili” kilicho upande wa juu kulia ili kusoma makala kamili.

Tanga – Jeshi la Polisi Mkoa wa Tanga linamshikilia mwanamke mmoja aitwaye Habiba Seleman Fundi kwa tuhuma za kumuiba mtoto mchanga katika Hospitali ya Wilaya ya Lushoto.

Akizungumza kuhusu tukio hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Almachius Mchunguzi, alisema mtuhumiwa alikamatwa Juni 21, 2026, majira ya saa 1:00 usiku katika Kitongoji cha Garekaya, Wilaya ya Lushoto, akiwa na mtoto huyo.

Kwa mujibu wa Kamanda Mchunguzi, tukio hilo lilianza Juni 19, 2026, majira ya saa 11:00 jioni, baada ya mama mzazi wa mtoto huyo, Mwanaidi Juma Nyaki, mkazi wa Kijiji cha Kwemakame, kutoa taarifa polisi kuwa mtoto wake mwenye umri wa siku moja alikuwa ametoweka akiwa amelazwa hospitalini.

Uchunguzi wa awali umebaini kuwa mtuhumiwa alijenga ukaribu na mama wa mtoto pamoja na ndugu waliokuwa wakimhudumia hospitalini, hatua iliyompa nafasi ya kupata imani yao.Endelea Kusoma Kwa Kubofya Hapa.

Post a Comment

Previous Post Next Post