Tafadhali Zingatia: Ikiwa unasoma kwenye PHOENIX, tafadhali bofya kitufe cha “Soma Makala Asili” kilicho upande wa juu kulia ili kusoma makala kamili.
Serikali imetangaza kuanza hatua mpya za kusafisha sekta ya madini kwa kufuta leseni ambazo hazitumiki, hatua inayolenga kupunguza udalali na kuhakikisha rasilimali za nchi zinatumika kwa tija. Kauli hiyo imeibua mjadala kuhusu mustakabali wa uwekezaji katika sekta yenye mchango mkubwa kwenye uchumi wa Tanzania.
Waziri wa Madini, , amesema Serikali haitasita kuchukua hatua dhidi ya wamiliki wa leseni za madini wanaoshindwa kuendeleza maeneo waliyopewa kwa ajili ya shughuli za uchimbaji. Amesema hatua hiyo inalenga kutoa nafasi kwa wawekezaji wenye uwezo wa kifedha, teknolojia na mipango madhubuti ya kuendesha miradi ya madini.
Akizungumza jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi rasmi wa Mkutano wa Saba wa Madini na Uwekezaji Tanzania, Mavunde alisema Serikali imejipanga kuhakikisha sekta ya madini inakuwa na ufanisi zaidi kupitia matumizi bora ya maeneo yenye rasilimali. Mkutano huo unatarajiwa kufanyika Novemba 19 hadi 21 katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC).
Kwa muda mrefu, changamoto ya baadhi ya wawekezaji kushikilia leseni bila kuendeleza shughuli imekuwa ikitajwa kama kikwazo katika ukuaji wa sekta ya madini. Serikali inaona hali hiyo inazuia wawekezaji wengine wenye uwezo kuingia na kuanzisha miradi yenye tija.Endelea Kusoma Kwa Kubofya Hapa.

Post a Comment