Iran imeweka masharti sita mazito kwa Marekani, ikisema utekelezaji wa masharti hayo ni muhimu kabla ya kuruhusu kufunguliwa kikamilifu kwa Mlango-Bahari wa Hormuz.
Msimamo huo umetolewa wakati mvutano kati ya Tehran na Washington ukiendelea kuibua hofu kuhusu usalama wa njia hiyo muhimu ya kimataifa ya usafirishaji wa mafuta.
Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Iran, Mohammad Baqer Zolqadr, amesema Iran inamtaka Rais wa Marekani, Donald Trump, kutimiza masharti hayo kama sehemu ya hatua za kupunguza mvutano.

Sharti la kwanza ni Marekani kukomesha vitisho na matusi dhidi ya Iran na mambo ambayo Tehran inayachukulia kuwa matakatifu.
Iran pia imemtaka Marekani kusitisha uchokozi wa kijeshi dhidi yake pamoja na washirika wake katika Lebanon, Palestina, Yemen na Iraq.

Tehran imesema hatua hiyo ni muhimu ili kuondoa mazingira yanayoweza kuchochea mapigano mapya katika Mashariki ya Kati.
Sharti la tatu ni kuondolewa kwa vikosi vya kijeshi vya Marekani vilivyopo karibu na mipaka ya Iran. Aidha, Iran inataka Marekani kulipa fidia kamili kwa hasara ambazo Tehran inadai zimesababishwa na vita dhidi ya taifa hilo.
Katika eneo la uchumi, Iran inataka vikwazo vyote vya kiuchumi dhidi ya wananchi wake viondolewe. Tehran imekuwa ikipinga vikwazo hivyo kwa muda mrefu, ikidai vinaathiri uchumi wake na maisha ya wananchi wake.
Sharti la mwisho ni kurejeshwa kwa mali zote za Iran zilizotaifishwa au kuzuiwa na Marekani, bila masharti.

Msimamo huu unaongeza uzito wa mvutano kuhusu Hormuz, njia ambayo ina umuhimu mkubwa katika biashara ya nishati duniani.
Sasa macho yanaelekezwa Washington kuona kama itajibu masharti hayo ya Tehran na kama hatua hiyo inaweza kufungua njia ya kupunguza mvutano katika eneo hilo.
Post a Comment