Jeshi la Anga la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu wa Iran (IRGC Aerospace Force) limedai kutekeleza shambulizi la pamoja dhidi ya Kituo cha Anga cha Muwaffaq Salti (Al-Azraq) nchini Jordan, ambacho Iran inasema kinatumiwa na vikosi vya Marekani kwa shughuli za kijeshi katika eneo la Mashariki ya Kati.
Kwa mujibu wa taarifa ya IRGC, operesheni hiyo ilianza kwa kutumia ndege zisizo na rubani za kujitoa mhanga aina ya Shahed-136, ambazo zilidaiwa kutumwa ili kulemea mifumo ya ulinzi wa anga ya kituo hicho.

Baada ya hatua hiyo, Iran inasema ilirusha makombora ya balistiki aina ya Fattah, Kheibar Shekan na Ghadr kuelekea malengo mbalimbali ndani ya kambi hiyo.
IRGC imedai kuwa mashambulizi hayo yalilenga maeneo yanayotumiwa na wanajeshi wa Marekani, mabanda ya kuhifadhi ndege za kivita pamoja na vituo vya amri na udhibiti wa operesheni za kijeshi.
IRGC imedai kuwa mashambulizi hayo yalilenga maeneo yanayotumiwa na wanajeshi wa Marekani, mabanda ya kuhifadhi ndege za kivita pamoja na vituo vya amri na udhibiti wa operesheni za kijeshi.
Iran imeeleza kuwa operesheni hiyo ilikuwa sehemu ya hatua za kulipiza kisasi kufuatia mashambulizi ambayo inadai Marekani ilifanya dhidi ya miundombinu ya Iran katika Kisiwa cha Qeshm kilichopo katika Mlango wa Hormuz.
Post a Comment