Jeshi la Marekani limeanza rasmi mchakato wa kuondoa vikosi vyake vilivyosalia nchini Iraq, hatua ambayo imeibua mijadala ya kisiasa na kijeshi katika eneo hilo.
Askari waliokuwa wakilinda maeneo ya kimkakati karibu na Uwanja wa Kimataifa wa Erbil katika mkoa wa Kurdistan wameanza kuondoka, sambamba na kuondolewa kwa mifumo ya ulinzi wa anga ya Patriot.
Hatua hii inatajwa kuwa sehemu ya utekelezaji wa makubaliano ya mwaka 2024 yaliyosainiwa kati ya Baghdad na Washington, yanayolenga kupunguza uwepo wa kijeshi wa Marekani nchini Iraq.
Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya kikanda, kuondoka kwa vikosi hivi kunakuja kabla ya tarehe ya mwisho ya Septemba 30, na kunahusishwa pia na mashambulio makubwa yaliyofanywa na Iran dhidi ya kambi ya kijeshi ya Erbil.

Wachambuzi wa usalama wanasema hatua hii inaweza kubadilisha mizani ya nguvu katika eneo, hasa ikizingatiwa jukumu la Marekani katika kupambana na makundi yenye misimamo mikali.
Post a Comment