Marekani Yaripotiwa Kutuma Tani 90,000 za Silaha Nchini Israel

Taarifa mpya kutoka Wizara ya Ulinzi ya Israel zinaonyesha kuwa Marekani imefikisha nchini humo silaha na vifaa vya kijeshi kupitia zaidi ya shehena 940 zilizosafirishwa kwa njia ya anga na bahari tangu kuanza kwa operesheni za kijeshi.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, usafirishaji huo umehusisha zaidi ya ndege 800 za mizigo pamoja na zaidi ya meli 140 za usafiri wa kijeshi. 

Miongoni mwa vifaa vilivyowasilishwa ni zaidi ya vipande 15,000 vya mabomu pamoja na zaidi ya makombora 57,000 ya mizinga ya milimita 155.

Inakadiriwa kuwa jumla ya tani zaidi ya 90,000 za silaha na vifaa vya kijeshi vilivyotumwa kutoka Marekani vina thamani ya kati ya dola bilioni 21.7 hadi takribani dola bilioni 30 za Marekani.

Misaada hiyo mikubwa ya kijeshi inaendelea kuwasili wakati juhudi za kimataifa za kusaka usitishaji wa mapigano na suluhisho la kidiplomasia katika eneo la Mashariki ya Kati zikiendelea kujadiliwa.


Post a Comment

Previous Post Next Post