Uteuzi Wa Rezaei kuwa Mwakilishi Wa Khamenei Katika Baraza kuu la Usalama Waikosesha Amani Israel

Israel imeonekana kuwa na wasiwasi mkubwa kufuatia hatua ya Kiongozi Mkuu wa Iran, Ayatollah Mojtaba Khamenei, kumteua Meja Jenerali Mohsen Rezaei kuwa mwakilishi wake katika Baraza Kuu la Usalama wa Taifa la Iran, chombo muhimu kinachohusika na masuala ya usalama wa taifa, sera za kijeshi na mikakati ya nje ya nchi.

Uteuzi huo ulitangazwa Jumapili, Agosti 9, 2026, na unamuweka Rezaei katika nafasi yenye ushawishi mkubwa katika maamuzi ya usalama wa Iran. Aidha, kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na vyombo vya habari, Rezaei ameteuliwa pia kuwa Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa baada ya Mohammad Bagher Zolghadr kujiuzulu Katika nafasi hiyo.

Mohsen Rezaei si mgeni katika masuala ya kijeshi na usalama wa Iran. Aliwahi kuwa kamanda wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) na kwa muda mrefu amekuwa akihusishwa na sera za kijeshi na kiusalama za Iran. Uzoefu wake wa muda mrefu ndani ya mfumo wa kijeshi unafanya uteuzi wake kuonekana kuwa na uzito mkubwa, hasa wakati Iran ikiwa katika kipindi cha mvutano mkubwa wa kikanda.

Kwa mujibu wa taarifa ya uteuzi huo, Khamenei alimchagua Rezaei akizingatia uzoefu wake mkubwa, hususan nafasi aliyowahi kushikilia wakati wa Vita vya Iran na Iraq. Uteuzi huo unaonyesha umuhimu ambao uongozi wa Iran unaendelea kuupa uzoefu wa kijeshi katika taasisi zake kuu za usalama. SOMA ZAIDI.

Post a Comment

Previous Post Next Post