Mvutano kati ya Israel na kundi la Hezbollah umeingia katika hatua mpya ya hatari baada ya Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu kutangaza kuwa mashambulizi dhidi ya kundi hilo yataongezwa zaidi.
Kwa upande wake, kundi la Hezbollah linaloungwa mkono na Iran lilitangaza kuwa limejibu mashambulizi hayo kwa kurusha makombora pamoja na droni kuelekea kaskazini mwa Israel.
Kauli hiyo imekuja wakati jeshi la Israel likisema tayari limeanzisha wimbi jipya la mashambulizi katika maeneo mbalimbali ya Lebanon, hasa Bonde la Bekaa pamoja na kusini mwa nchi hiyo.
Kwa mujibu wa Jeshi la Ulinzi la Israel (IDF), zaidi ya maeneo 100 yanayodaiwa kutumiwa na wapiganaji wa Hezbollah yalilengwa ndani ya muda mfupi.

Mashambulizi hayo yaliripotiwa kujumuisha maghala ya silaha, vituo vya mawasiliano pamoja na maeneo yanayodhaniwa kutumika kurushia roketi kuelekea Israel.
Vyombo vya habari vya Lebanon viliripoti kuwa watu wasiopungua 12 waliuawa katika kijiji cha Mashghara baada ya mashambulizi makubwa ya anga kufanywa usiku wa Jumanne.

Wakazi wengi walionekana wakikimbia makazi yao huku milio ya milipuko ikisikika katika maeneo mbalimbali ya kusini mwa Lebanon.
Kwa upande wake, kundi la Hezbollah linaloungwa mkono na Iran lilitangaza kuwa limejibu mashambulizi hayo kwa kurusha makombora pamoja na droni kuelekea kaskazini mwa Israel.
Kundi hilo lilisema lililenga wanajeshi wa Israel, vifaru, vituo vya kijeshi pamoja na miundombinu ya kijeshi katika operesheni 22 tofauti.
Kauli ya Netanyahu kwamba Israel “iko vitani na Hezbollah” imeongeza zaidi hofu ya kuzuka kwa vita vikubwa katika eneo lote la Mashariki ya Kati.

Waziri huyo alisema jeshi lake limewaua zaidi ya wapiganaji 600 wa Hezbollah katika wiki za hivi karibuni, lakini akaongeza kuwa hatua hiyo haitoshi na kwamba “nguvu ya mashambulizi lazima iongezwe sasa.”
Kauli hiyo imeungwa mkono na baadhi ya mawaziri wenye msimamo mkali ndani ya serikali ya Israel akiwemo Itamar Ben-Gvir pamoja na Bezalel Smotrich ambao wametaka operesheni za kijeshi ziongezwe hadi mji mkuu wa Lebanon, Beirut.
Hata hivyo, hali hiyo imeibua wasiwasi mkubwa kimataifa hasa kutokana na ukweli kwamba mwezi huu Israel na Lebanon zilikuwa zimekubaliana kuongeza muda wa usitishaji wa mapigano kwa siku nyingine 45.

Ingawa makubaliano hayo yalitarajiwa kupunguza vurugu mpakani, mashambulizi yameendelea karibu kila siku huku kila upande ukiilaumu mwingine kwa kuvunja makubaliano hayo.
Wachambuzi wa masuala ya usalama wanasema kuongezeka kwa mashambulizi ya Israel kunaweza kuwa sehemu ya mkakati wa kuzuia Hezbollah kuimarisha uwezo wake wa kijeshi, hasa matumizi ya droni mpya za kisasa zinazotumia teknolojia ya fiber optic ambazo zimeripotiwa kutumika kushambulia majeshi ya Israel kusini mwa Lebanon.
Wataalamu hao wanaamini kuwa teknolojia hiyo imeipa Hezbollah uwezo mkubwa wa kufanya mashambulizi ya kushtukiza bila kugundulika kwa urahisi.

Hali hiyo imeongeza changamoto kubwa kwa mifumo ya ulinzi ya Israel ambayo kwa miaka mingi imekuwa ikitegemewa kulinda mipaka yake dhidi ya mashambulizi kutoka nje.
Zaidi ya hayo, wachambuzi wa siasa za Mashariki ya Kati wanaona mgogoro huo sasa ukiwa umeunganishwa moja kwa moja na mvutano mpana unaohusisha Iran, Marekani pamoja na Israel.

Serikali ya Iran imekuwa ikisisitiza kuwa mazungumzo yoyote ya amani lazima yajumuishe kusitishwa kwa mapigano katika maeneo yote yenye vita katika ukanda huo.
Kwa upande mwingine, serikali ya Israel haijaonyesha dalili yoyote ya kusitisha operesheni zake dhidi ya Hezbollah.

Rais wa Lebanon Joseph Aoun ameendelea kuitaka Israel kuondoa wanajeshi wake kusini mwa Lebanon akisema uwepo wa vikosi hivyo unaendelea kuchochea mapigano.
Wakati huo huo, mamia ya maelfu ya wananchi wa Lebanon wameendelea kuyakimbia makazi yao kwa hofu ya mashambulizi zaidi.

Hali hiyo imeongeza mgogoro wa kibinadamu huku hospitali na huduma za kijamii zikianza kupata shinikizo kubwa kutokana na ongezeko la majeruhi na wakimbizi wa ndani.
Wataalamu wa diplomasia wanaonya kuwa ikiwa mashambulizi yataendelea kuongezeka, kuna hatari kubwa ya kuzuka kwa vita kamili kati ya Israel na Hezbollah jambo ambalo linaweza kuathiri mataifa mengi ya Mashariki ya Kati.

Pia wanaeleza kuwa ushiriki wa Iran, moja kwa moja au kupitia makundi washirika wake, unaweza kuifanya vita hiyo kuwa kubwa zaidi kuliko inavyotarajiwa sasa.
Kadri mashambulizi yanavyoendelea, macho ya dunia sasa yameelekezwa katika mazungumzo yajayo yanayotarajiwa kufanyika Washington kati ya viongozi wa Israel na Lebanon, huku wengi wakisubiri kuona kama juhudi za kidiplomasia zitaweza kuzuia eneo hilo kuingia katika vita vipya vya muda mrefu.
TAZAMA VIDEO.

Post a Comment