Mdau wa maendeleo Adriano Bukombe ameibua mjadala mzito wa kisiasa na kijamii kuhusu umaarufu na mvuto wa Waziri Mkuu wa Tanzania, Mwigulu Nchemba, akieleza namna ambavyo kiongozi huyo ameibuka kuwa kipenzi cha wananchi wa hali ya chini, maarufu kama “wanyonge”.
Katika maelezo yake, Bukombe anasisitiza kuwa haijalishi mtu anampenda au hampendi Mwigulu, lakini hali halisi inaonesha wazi kuwa kuna kundi kubwa la Watanzania linaonesha imani kubwa kwake kwa vitendo.
Kwa mujibu wa mdau huyo, hali ya wananchi kusafiri kutoka maeneo mbalimbali ya nchi kumfuata Waziri Mkuu huyo si jambo la kawaida katika historia ya Tanzania.
Kwa mujibu wa mdau huyo, hali ya wananchi kusafiri kutoka maeneo mbalimbali ya nchi kumfuata Waziri Mkuu huyo si jambo la kawaida katika historia ya Tanzania.
Analinganisha mvuto huo na ule wa viongozi wa kiroho kama madaktari, wahubiri au waganga, akimaanisha kuwa watu wanamfuata Mwigulu wakiwa na matarajio makubwa ya kupata suluhisho la changamoto zao.
Jambo la msingi analosisitiza ni kuwa matarajio hayo mara nyingi yanapata majibu, jambo linaloongeza imani yao kwake.
Post a Comment