Hii Ndio Adhabu ya Tundu Lissu Julai 6 Kama Akikutwa na Hatia Kwenye Kesi ya Uhaini

DAR ES SALAAM – Hali ya sintofahamu na presha kubwa ya kisiasa imeendelea kutikisa taifa kufuatia uamuzi wa Mahakama ya Rufaa kuahirisha tena usikilizwaji wa shauri linalomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA, Mhe. 

Tundu Antipas Lissu, huku hatma yake sasa ikitarajiwa kujulikana Julai 6, 2026.

Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa, shauri hilo la Maombi ya Jinai Na. 7440840/2026 kati ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) na Tundu Lissu limepangiwa kutolewa uamuzi, hukumu au amri rasmi (Judgments, Rulings & Orders) katika tarehe hiyo mpya, hatua inayozidisha mjadala mkali wa kitaifa kuhusu mwenendo wa kesi hiyo nyeti.

Taarifa hiyo imepokelewa kwa hisia kali miongoni mwa wafuasi wa CHADEMA na wananchi wanaofuatilia kwa karibu kesi hiyo, wengi wakieleza hofu na maswali mazito kuhusu mustakabali wa kiongozi huyo wa upinzani na mwelekeo wa haki nchini.S.O.M.A Z.A.ID.I.

Post a Comment

Previous Post Next Post