Iran Yazipa Onyo Marekani Na Israel.Isijaribu Kuishambulia Kwenye Miundombinu Yao Watajuta

Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imeongeza tahadhari dhidi ya Marekani na Israel, ikitoa onyo kali kuhusu uwezekano wa mashambulizi yanayolenga miundombinu yake ya nishati. 

Kupitia jeshi lake la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC), Tehran imesisitiza kuwa hatua yoyote ya kijeshi itakabiliwa na majibu makali na yenye maumivu.

Afisa wa usalama wa Iran ameliambia shirika la habari la Tasnim kwamba taifa hilo limeandaa mpango kamili wa kujibu uzembe wowote wa Marekani au washirika wake. Onyo hilo limeeleza kuwa majibu yatakuwa na athari kubwa kwa taifa la Kiyahudi na maeneo yote yenye maslahi ya Marekani katika Mashariki ya Kati. SOMA ZAIDI.

Post a Comment

Previous Post Next Post