IDF Yaishambulia Iran Baada ya Shambulio la Makombora Kutoka Tehran

Mvutano kati ya Israel na Iran umeendelea kuongezeka kwa kasi kubwa baada ya taarifa mpya kueleza kuwa Jeshi la Ulinzi la Israel (IDF) limefanya mashambulizi katika maeneo ya magharibi na kati mwa Iran. 

Hatua hiyo inaripotiwa kuja muda mfupi baada ya Iran kuishambulia Israel kwa kurusha makombora ya masafa marefu (ballistic missiles).

Kwa mujibu wa taarifa hizo za awali kutoka vyombo mbalimbali vya habari vya kimataifa, mashambulizi ya Israel yanalenga maeneo yanayodaiwa kuwa na miundombinu ya kijeshi ndani ya Iran. 

Hata hivyo, bado hakuna uthibitisho wa kina kuhusu kiwango cha uharibifu au majeruhi waliotokana na mashambulizi hayo.

Wakati huohuo, Iran iliripotiwa kuanzisha mashambulizi ya makombora dhidi ya Israel kama sehemu ya kulipiza kisasi, hali iliyochochea mzunguko mpya wa mashambulizi kati ya pande hizo mbili zinazozidi kuwa na uhasama wa muda mrefu. Hali hii imeongeza wasiwasi mkubwa katika eneo la Mashariki ya Kati.

Post a Comment

Previous Post Next Post