Dar es Salaam, Juni 2026 — Mwanasiasa na aliyewahi kuwa Mbunge wa Iringa Mjini, Peter Msigwa, amezua mjadala mkubwa baada ya kueleza tofauti aliyoiona kati ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), akisema kuwa wakati akiwa ndani ya CCM kulikuwa na posho kwa shughuli mbalimbali za chama, hali ambayo amesema haipo ndani ya Chadema.
Akizungumza katika mahojiano na mwanahabari Chief Odemba katika kipindi cha Medani Kuu, Msigwa alisema kuwa moja ya tofauti alizoziona baada ya kurejea Chadema ni suala la posho zinazotolewa kwa wanachama au viongozi wanapopewa majukumu maalumu.
"Kule CCM ukipewa mission kulikuwa na posho. Huku Chadema mambo hayo hayapo," alisema Msigwa wakati wa mahojiano hayo, kauli ambayo imeibua mijadala mbalimbali miongoni mwa wadau wa siasa nchini.
Kauli hiyo ilizua maswali kuhusu sababu halisi zilizomfanya kurejea Chadema baada ya kuondoka na kujiunga na CCM kwa kipindi cha takribani miaka miwili.

Wapo waliotafsiri maneno yake kama ishara kwamba mazingira ya kisiasa ndani ya vyama hivyo viwili yana tofauti kubwa katika namna ya uendeshaji wa shughuli zao za kila siku. SOMAZ ZAIDI.
Post a Comment