DUBAI/CAIRO — Rais wa Marekani Donald Trump amesema amefanya mazungumzo yenye mafanikio na Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu pamoja na wawakilishi wa Hezbollah kupitia wapatanishi, hatua ambayo imeongeza matumaini ya kudumu kwa usitishaji wa mapigano nchini Lebanon licha ya kuendelea kwa mvutano wa kikanda. TAZAMA VIDEO.
Kupitia ujumbe aliouchapisha kwenye jukwaa lake la Truth Social Jumatatu, Trump alisema mazungumzo hayo yalizaa makubaliano ya awali yanayolenga kuzuia kuongezeka kwa mapigano kati ya Israel na Hezbollah.
Rais huyo alisema amepata uhakikisho kwamba vikosi vya Israel havitaelekea mji mkuu wa Lebanon, Beirut, na kwamba wanajeshi waliokuwa wakisogea kuelekea eneo hilo tayari wameagizwa kurejea nyuma.
“Hakutakuwa na wanajeshi wa Israel watakaoelekea Beirut, na wale waliokuwa njiani tayari wamerudishwa,” alisema Trump.
Aidha, Trump alidai kuwa Hezbollah kupitia wawakilishi wake imekubali kusitisha mashambulizi dhidi ya Israel, huku akieleza kuwa hatua hiyo inaweza kuwa mwanzo wa kurejea kwa utulivu katika eneo hilo ambalo limekumbwa na mapigano kwa miezi kadhaa.
“Nilikuwa na mazungumzo mazuri sana na Hezbollah kupitia wawakilishi wa ngazi za juu, na wamekubali kwamba mashambulizi yote yatasimama,” alisema.
Tangazo hilo lilikuja wakati ambapo juhudi za kidiplomasia katika Mashariki ya Kati zinakabiliwa na changamoto mpya baada ya vyombo vya habari vya serikali ya Iran kuripoti kwamba Tehran imeamua kusitisha mazungumzo yasiyo ya moja kwa moja na Marekani.
Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Tasnim la Iran, uamuzi huo ulitokana na hatua ya Israel kuamuru vikosi vyake kuendelea kusonga ndani ya Lebanon na kuongeza operesheni za kijeshi dhidi ya Hezbollah.
Hatua hiyo imeibua wasiwasi kwamba juhudi za kimataifa za kumaliza vita vilivyodumu kwa takribani miezi mitatu zinaweza kukwama ikiwa kutakuwa na kuongezeka kwa mapigano nchini Lebanon.
Hata hivyo, Trump alisema hakuwa amepokea taarifa rasmi kutoka Tehran kuhusu kusitishwa kwa mazungumzo hayo.

Akizungumza na mwandishi wa NBC News, rais huyo alisema bado anaamini kuwa diplomasia inaweza kuendelea.
Post a Comment