Aliyekuwa Katibu wa CHADEMA, Barnabas Okolla, apinga kauli za John Mnyika Alizotoa Kuhusu Heche

Tafadhali Zingatia: Ikiwa unasoma kwenye PHOENIX, tafadhali bofya kitufe cha “Soma Makala Asili” kilicho upande wa juu kulia ili kusoma makala kamili.

Aliyekuwa Katibu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mkoa wa Morogoro, Barnabas Okolla, amesema amesikitishwa na kauli zilizotolewa na Katibu Mkuu wa chama hicho, John Mnyika, zinazodai kuwa baadhi ya wanachama wamepewa rushwa ya Sh milioni 2 ili kumchafua Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Bara, John Heche.

Akizungumza kuhusu suala hilo, Okolla amesema madai hayo ni mazito na yanapaswa kuthibitishwa kwa ushahidi badala ya kutolewa hadharani bila vielelezo. Amesisitiza kuwa hadi sasa hajawahi kupewa fedha hizo wala kushiriki njama yoyote ya kumchafua kiongozi yeyote wa chama.

Kwa mujibu wa Okolla, yeye kama mwanachama na kiongozi wa zamani wa CHADEMA ana haki ya kutoa maoni yake kuhusu mwenendo wa chama na masuala yanayohusu uongozi wake. Amesema maoni aliyoyatoa yalikuwa sehemu ya wajibu wake wa kisiasa na yalilenga kuhimiza uwajibikaji ndani ya chama.Endelea Kusoma Kwa Kubofya Hapa.

Post a Comment

Previous Post Next Post