Kumbe Huyu ndiye Mwizi aliyekamatwa Baada ya kuvamia Benki

Tafadhali Zingatia: Ikiwa unasoma kwenye PHOENIX, tafadhali bofya kitufe cha “Soma Makala Asili” kilicho upande wa juu kulia ili kusoma makala kamili.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Kipolisi Tarime/ Rorya kupitia kwa Kamanda wake Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi Mark Njera ameseme picha Mjongeo inayosambazwa Mtandaoni ikimuonesha Askari Polisi akipambana na mtu mmoja, imetokana na tukio la mtu huyo (John Kohe Amos) kuvamia Benki ya CRDB tawi la Sirari na kuamuru kupewa fedha bila kufuata taratibu.

Kamanda Njera katika taarifa yake kwa vyombo vya habari leo alhamis 2025 amesema katika tukio hilo la Julai 2,2026, Mtu huyo Mkazi wa Kijiji cha Sokoni– Sirari, alifika katika benki hiyo saa nane mchana na kuingia ndani na kwenda kwa mtoa huduma wa benki (bankteller) kama mteja huku akiwa amebeba begi dogo na kumwamuru kwa nguvu mtoa huduma ampe fedha bila kufuata taratibu za kibenki.

Taarifa ya Polisi imesema hali hiyo ilisababisha wasiwasi ndani ya Benki hiyo na kulazimu Askari Polisi waliokuwa lindo nje ya Benki hiyo kuitwa na baadae kumfuata mtu huyo na kumtaka atoke nje, suala ambalo alitii na walipofika nje akafanya jaribio la kumnyang’anya Askari Polisi silaha yake ya moto ili kupambana naye.Endelea Kusoma Kwa Kubofya Hapa.

Post a Comment

Previous Post Next Post