Top News

Polisi Wachunguza Kifo Cha Dereva Wa John Heche Watoa Majibu Haya

Tafadhali Zingatia: Ikiwa unasoma kwenye PHOENIX, tafadhali bofya kitufe cha “Soma Makala Asili” kilicho upande wa juu kulia ili kusoma makala kamili.

Jeshi la Polisi mkoani Kigoma limeanzisha uchunguzi wa kina kufuatia kifo cha Suezi Maradufu, aliyekuwa dereva wa Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), John Heche, ambaye alikutwa amefariki katika nyumba ya kulala wageni.

Kwa mujibu wa taarifa za awali kutoka kwa Jeshi la Polisi, tukio hilo liligundulika baada ya askari kufika eneo la tukio kufuatia taarifa za mashaka kutoka kwa watu waliokuwa karibu na nyumba hiyo ya kulala wageni. Baada ya kufika, polisi walilazimika kuvunja mlango wa chumba alichokuwa akiishi marehemu ili kuingia ndani.

Ndani ya chumba hicho, walimkuta Suezi Maradufu akiwa amelala sakafuni kifudifudi bila dalili za uhai. Uchunguzi wa haraka wa eneo la tukio ulifanyika mara moja ili kubaini mazingira ya kifo hicho, ambapo polisi waligundua uwepo wa vidonge vya aina mbalimbali ndani ya chumba hicho.Endelea Kusoma Kwa Kubofya Hapa.

Post a Comment

Previous Post Next Post