Aliyemshika Mwanamke Sehemu za Siri Apigwa Risasi Mara 14

Taarifa iliyotolewa tarehe 7 julai 2026, Mwanadada Alishon Torres, mwenye umri wa miaka 18, ameibua mjadala mkubwa baada ya kufikishwa mahakamani mjini Memphis kwa tuhuma za mauaji ya makusudi. 

Kesi hii imevuta hisia za wengi kutokana na mazingira yaliyosababisha tukio hilo. Kwa mujibu wa upande wa mashtaka, Torres alimpiga risasi Noe Rincon mara kadhaa, ikiwemo moja kwenye paji la uso, baada ya kusikia madai kwamba Rincon alimshika dada yake mdogo wa miaka mitano sehemu za siri. 

Tukio hili lilitokea ndani ya gari la mizigo, ambalo baadaye lilipakwa rangi na kutelekezwa ili kuficha ushahidi.  

Polisi walibaini kuwa Torres alitupa silaha ya pili, lakini bastola ya kiwango cha .40 ilipatikana akiwa nayo wakati wa kukamatwa. 

Hali hii imeongeza uzito wa mashtaka dhidi yake, ikiwemo kuharibu ushahidi na kutumia silaha ya moto katika kutenda kosa lenye hatari. 

Upande wa utetezi umeeleza kuwa Torres ni mhamiaji kutoka Honduras mwenye elimu ya darasa la tano tu, na kwamba alikuwa amechanganyikiwa sana kiakili wakati wa kuhojiwa. 

Wanasheria wake wanapendekeza mahakama izingatie hali yake ya kisaikolojia na mazingira yaliyomfanya kutoa kauli zinazoweza kumtia hatiani. SOMA ZAIDI.

Post a Comment

Previous Post Next Post