Kocha Mpya Yanga Amkataa Mchezaji Huyu Tegemeo

Kocha mpya wa yanga baada ya kutua kikosini ameomba CV za Kila mchezaji wale aliowakuta na kukagua. 

Majibu yaliyotoka ni kwamba licha ya maboresho makubwa ambayo yanga wamefanya ila Kuna sehemu pia inatakiwa yafanyike mabadiliko ili kikosi kiweze kuleta mafanikio

Changamoto alizoziona kwa diarra ni makosa ya kujirudiarudia ya kinidhamu ambapo kocha huyo amewaambia yanga mpira unahitaji nidhamu kwanza kuliko kitu chochote hivyo kwa diarra ni wazi hana nidhamu hivyo hatuwezi kuwa na mchezaji w aina yake kama kweli tunahitaji mafanikio.

Mngqithi, anayejulikana kwa falsafa ya soka la kushambulia lenye nidhamu ya hali ya juu, ameweka wazi kuwa mafanikio ya Yanga katika mashindano ya ndani na kimataifa yatategemea uimara wa safu ya ulinzi na kiungo cha kati. Kwa mtazamo wake, beki wa kati imara atasaidia kuimarisha safu ya ulinzi dhidi ya mashambulizi ya wapinzani, huku kiungo mkabaji akihitajika kuunganisha ulinzi na mashambulizi kwa kasi na usahihi.

Mashabiki wa Yanga walipokea taarifa hizi kwa shangwe kubwa, wakimtaja Mngqithi kama “kocha mwenye maono mapya” wa Jangwani. Mitandaoni, mjadala ulilipuka kwa kasi, mashabiki wakieleza kuwa Yanga imeonyesha mfano wa klabu yenye mikakati ya muda mrefu na inayojua namna ya kuimarisha kikosi chake kwa wachezaji wenye nidhamu na uwezo wa kiufundi. Wengi walisisitiza kuwa mapendekezo ya kocha mpya ni ishara ya Yanga kuendelea kujipanga kwa ushindani wa ndani na kimataifa.


Post a Comment

Previous Post Next Post