Yanga Hoi Baada ya Kupokea Barua Hii Kutoka FIFA

Young Africans SC (Yanga) wamejikuta katika hali ya dharura baada ya kupokea barua rasmi kutoka FIFA ikiwazuia kusajili wachezaji wapya kwa madirisha matatu mfululizo kuanzia Agosti 5, 2026. 

Hatua hii imekuwa pigo kubwa kwa klabu hiyo, ambayo imekuwa ikijipanga kuimarisha kikosi chake kuelekea msimu mpya wa Ligi Kuu NBC na mashindano ya kimataifa.

Adhabu hii imetokana na madeni ambayo klabu inapaswa kulipa kabla ya kuendelea na usajili. Kwa mujibu wa taratibu za FIFA, klabu yoyote inayoshindwa kutekeleza majukumu yake ya kifedha kwa wachezaji, makocha au klabu nyingine inaweza kufungiwa kusajili hadi pale itakapokamilisha malipo husika. 

Hali hii imeweka Yanga katika mazingira magumu, kwani kushindwa kusajili kwa misimu mitatu kutamaanisha kikosi chao kitategemea wachezaji waliopo bila kuongeza nguvu mpya.

Post a Comment

Previous Post Next Post