CCM Yafanya Mabadiliko Sekretarieti, Mwanri Ateuliwa Naibu Katibu Mkuu

Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimefanya mabadiliko katika muundo wa Sekretarieti yake baada ya Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa kufanya uteuzi wa viongozi wapya katika nafasi mbalimbali za uongozi.

Mabadiliko hayo yaliyofanyika Zanzibar yamelenga kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa majukumu ya chama, huku baadhi ya viongozi wakipewa dhamana mpya na wengine kuendelea na nafasi zao kwa ajili ya kudumisha mwendelezo wa shughuli za chama.

Katika mabadiliko hayo, Agrey Mwanri ameteuliwa kuwa Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara, akichukua nafasi iliyokuwa ikishikiliwa na John Mongella.

Mwanri ana uzoefu wa muda mrefu katika masuala ya uongozi wa kisiasa na serikali, ambapo anatarajiwa kutumia uzoefu huo kuimarisha shughuli za chama katika maeneo mbalimbali ya Tanzania Bara.


Post a Comment

Previous Post Next Post